Mark 2:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Watu hawakati kiraka cha nguo mpya na kukishonea katika nguo kuukuu. Kama wakifanya hivyo, hicho kiraka kipya kitararuka kutoka hilo vazi kuukuu, nalo litaharibika zaidi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Hakuna mtu ashoneaye kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, kile kiraka kipya kitachanika kutoka ile nguo iliyochakaa, nayo itachanika zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipotatuka huzidi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hakuna anayeshona kiraka kipya cha nguo kwenye vazi la zamani. Ikiwa atafanya hivyo kiraka hicho kipya kitajikunjakunja na kulinyofoa vazi hilo zee nalo litachanika vibaya zaidi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Hakuna mtu anayekata kiraka kutoka katika nguo mpya na kukishonea katika nguo kuukuu. Kama akifanya hivyo, hicho kiraka kipya kitararuka kutoka hilo vazi kuukuu, nalo litaharibika zaidi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Watu hawakati kiraka cha nguo mpya na kukishonea katika nguo kuukuu. Kama wakifanya hivyo, hicho kiraka kipya kitararuka kutoka hilo vazi kuukuu, nalo litaharibika zaidi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Hakuna mtu ashoneaye kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, kile kiraka kipya kilichoshonewa kwenye nguo iliyochakaa huondoka, nayo ile nguo huchanika zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Hakuna mtu ashoneaye kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, kile kiraka kipya kitachanika kutoka ile nguo iliyochakaa, nayo itachanika zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; akishona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipotatuka huzidi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Watu hawakati kiraka cha nguo mpya na kukishonea katika nguo kuukuu. Kama wakifanya hivyo, hicho kiraka kipya kitararuka kutoka hilo vazi kuukuu, nalo litaharibika zaidi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuna mtu anayetia kiraka cha nguo mpya katika kanzu chakavu; kama anafanya hivyo, kile kiraka kipya kinaondoa pote paliposhonwa katika kanzu chakavu; hivyo tundu lake litakuwa kubwa zaidi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipotatuka huzidi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Hakuna mutu anayeshonea kiraka kipya juu ya nguo ya zamani. Kama akifanya vile, kile kiraka kipya kinapasua nguo ya zamani, nako kupasuka kwake kunaongezeka zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hakuna mtu ashonae kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu: ikiwa ashona, kile kipya kilicholiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipolatuka huzidi.