Mark 2:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano. Walipokuwa wanatembea, wanafunzi wake wakaanza kukata masuke ya ngano.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku moja ya Sabato, Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakipita katikati ya mashamba ya nafaka. Walipokuwa wakitembea, wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato, wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikatokea kwamba katika siku ya Sabato Yesu na wanafunzi wake walikuwa wakipita katika mashamba ya nafaka. Wanafunzi wake walianza kuchuma masuke ya nafaka ile walipopita.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano. Walipokuwa wanatembea, wanafunzi wake wakaanza kukwanyua masuke ya ngano.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano. Walipokuwa wanatembea, wanafunzi wake wakaanza kukata masuke ya ngano.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku moja ya Sabato, Yesu pamoja na wanafunzi wake, walikuwa wakipita katikati ya mashamba ya nafaka. Walipokuwa wakipita wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku moja ya Sabato, Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wakipita katikati ya mashamba ya nafaka. Walipokuwa wakitembea, wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato, wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku moja ya Sabato, Yesu alikuwa anapita katika mashamba ya ngano. Walipokuwa wanatembea, wanafunzi wake wakaanza kukata masuke ya ngano.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawa akipita katika mashamba siku ya mapumziko; nao wanafunzi wake wakaanza kuendelea njiani wakikonyoa masuke.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato, wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja ya Sabato Yesu akapita katika mashamba ya ngano. Wanafunzi wake wakaanza kuchumachuma masuke ya ngano kwa kadiri walivyoendelea katika njia.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta alipokuwa akipita katika makonde siku ya sabato, wanafunzi wake wakaanza kuendelea wakivunja masuke.