Mark 2:26 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye aliingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani tu. Naye pia akawapa wenzake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiathari, akaila mikate ile ya Wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilikuwa wakati wa Abiathari Kuhani Mkuu. Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu na kula mkate uliotolewa kwa Bwana. Sheria ya Musa inasema ni makuhani peke yao ndio watakaoweza kuula mkate ule. Daudi aliwapa pia ule mkate mtakatifu watu waliokuwa pamoja naye.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
naye akaingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa Kuhani Mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye aliingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu wakati Abiathari akiwa Kuhani Mkuu, akaila ile Mikate Mitakatifu, ambayo ilikuwa hairuhusiwi mtu ye yote kuila isipokuwa makuhani, naye akawapa wenzake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu, akaila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu, akaila mikate ile ya wonesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye aliingia ndani ya Nyumba ya Mungu, akala ile mikate iliyowekwa mbele ya Mungu. Jambo hili lilifanyika wakati Abiathari alikuwa kuhani mkuu. Na ni makuhani tu peke yao waliokuwa wameruhusiwa kula mikate hiyo. Lakini Daudi aliila, tena akawapa na wenzake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo aliingia Nyumbani mwa Mungu kwa mtambikaji mkuu Abiatari, akaila mikate aliyowekewa Bwana, nayo kuila ni mwiko, huliwa na watambikaji tu; kisha akawapa nao wenziwe waliokuwa naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiathari, akaila mikate ile ya Wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Si aliingia ndani ya nyumba ya Mungu na kula mikate mitakatifu iliyotolewa kwa Mungu? Jambo hili lilifanyika wakati Abiatari alipokuwa Kuhani Mukubwa. Ni makuhani tu walioruhusiwa kula mikate ile, lakini Daudi alikula na kuwapa watu wake vilevile.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiatbar, akaila mikate iliyotolewa kwa Mungu, isiyo halali kuliwa illa na makuhani, akawapa na wenziwe?