Mark 2:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu ya huo umati wa watu, hawakuweza kumpeleka karibu na Yesu. Basi, wakatoboa sehemu ya paa iliyokuwa juu ya mahali alipokuwa Yesu. Walipokwisha pata nafasi, wakamteremsha huyo mtu akiwa amelala juu ya mkeka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa hawakuweza kumfikisha kwa Isa kwa sababu ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa juu ya mahali Isa alikuwa, wakamshusha mtu aliyepooza akiwa amelalia mkeka wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu hao hawakuweza kumfikisha mgonjwa kwa Yesu kwa sababu ya umati wa watu ulioijaza nyumba yote. Hivyo walipanda na kuondoa paa juu ya sehemu aliposimama Yesu. Baada ya kutoboa tundu darini kwenye paa, wakateremsha kirago alimokuwa amelala yule aliyepooza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kwa sababu ya huo umati wa watu, hawakuweza kumpeleka karibu na Yesu. Basi, wakatoboa sehemu ya dari iliyokuwa juu ya mahali alipokuwa Yesu. Walipokwisha pata nafasi, wakamteremsha huyo mtu akiwa amelala juu ya mkeka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu ya huo umati wa watu, hawakuweza kumpeleka karibu na Yesu. Basi, wakatoboa sehemu ya paa iliyokuwa juu ya mahali alipokuwa Yesu. Walipokwisha pata nafasi, wakamteremsha huyo mtu akiwa amelala juu ya mkeka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa walikuwa hawawezi kumfikisha kwa Yesu kwa ajili ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa mahali pale alipokuwa Yesu, wakamshusha yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa walikuwa hawawezi kumfikisha kwa Isa kwa ajili ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa mahali pale alipokuwa Isa, wakamshusha yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kulivunja wakaliteremsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu ya huo umati wa watu, hawakuweza kumpeleka karibu na Yesu. Basi, wakatoboa sehemu ya paa iliyokuwa juu ya mahali alipokuwa Yesu. Walipokwisha pata nafasi, wakamteremsha huyo mtu akiwa amelala juu ya mkeka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wasipoweza kumpelekea yeye kwa ajili ya watu wengi wakafumua paa hapo, alipokuwapo. Walipokwisha kupatoboa wakakishusha kitanda, alichokilalia yule mgonjwa wa kupooza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kwa kuona hawakuweza kumufikisha mbele ya Yesu kwa sababu ya uwingi wa watu, wakabomoa dari juu ya pahali Yesu alipokuwa. Kisha wakamushusha yule mwenye kupooza kwenye nafasi ile walipobomoa, akilala juu ya kipoyi chake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu va makutano, wakaitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakakitelemsha kitanda alichokilalia yule mwenye kupooza.