Mark 2:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni lipi lililo rahisi zaidi: Kumwambia mtu huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kumwambia, ‘Inuka! Chukua mkeka wako utembee?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uchukue mkeka wako, uende’?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakati akiwa duniani Mwana wa Adamu anayo mamlaka ya kusamehe dhambi. Lakini nitawezaje kulithibitisha hili kwenu? Pengine mnafikiri ilikuwa rahisi kwangu kumwambia mtu huyu aliyepooza ‘Dhambi zako zimesamehewa,’ kwa sababu hilo haliwezi kuthibitishwa kwamba hakika limetokea. Lakini vipi nikimwambia mtu huyu, ‘Simama! Beba kirago chako na utembee’?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia mtu huyu aliyepooza, Umesamehewa dhambi zako, au kumwambia, Inuka! Chukua mkeka wako utembee?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia mtu huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kumwambia, ‘Inuka! Chukua mkeka wako utembee?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni jambo gani lililo rahisi, kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uchukue kitanda chako uende’?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uchukue mkeka wako, uende’?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni lipi lililo rahisi zaidi: Kumwambia mtu huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kumwambia, ‘Inuka! Chukua mkeka wako utembee?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kilicho chepesi ni kipi? Kumwambia mwenye kupooza: Makosa yako yameondolewa! au kusema: Inuka, ukichukue kitanda chako, uende?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kitu gani kinachokuwa chepesi: kumwambia mutu mwenye kupooza ‘Zambi zako zimesamehewa’ au kumwambia ‘Simama, utwae kipoyi chako na utembee?’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Vipi vyepesi, kumwambia mwenye kupooza, Dhambi zako zimeondolewa, au kusema, Ondoka, njitwike kitanda chako, ukaenende?