Mark 3:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawatazama kwa hasira watu waliomzunguka pande zote, akahuzunika sana kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukawa umeponywa kabisa!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawatazama wote waliomzunguka kwa hasira lakini alihuzunika kwa sababu waliifanya mioyo yao kuwa migumu. Akamwambia mtu yule “nyosha mkono wako”, naye akaunyosha, na mkono wake ukapona.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia huyo mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawatazama pande zote kwa hasira, akahuzunika sana kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyosha mkono wako.” Akaunyosha, nao ukapona kabisa!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawatazama pande zote kwa hasira, akahuzunika sana kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukaponywa kabisa!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo akawatazama wote kwa hasira, akaona huzuni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Kisha akamwambia yule mtu, “Nyosha mkono wako!” Naye akaunyosha mkono wake, ukawa mzima tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ukali ukamjia, akawatazama waliokuwako, akausikitikia ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu: Unyoshe mkono wako! Alipounyosha, huo mkono wake ukageuka kuwa mzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawakazia macho kwa kasirani, akihuzunika kwa sababu ya ugumu wao. Akamwambia yule mutu: “Nyoosha mukono wako.” Akaunyoosha, nao ukakuwa muzima tena.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawakazia macho pande zote kwa ghadhabu, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu. Nyosha mkono wako. Akaunyosha: mkono wake ukapona ukawa mzima kama wa pili: