Mark 3:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Idumea, ngambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, makundi ya watu wakamjia kutoka Yudea, Yerusalemu, Idumaya, na ng’ambo ya Yordani, pamoja na wale wa maeneo ya Tiro na Sidoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na Yerusalemu, na Idumaya, na ng'ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yerusalemu, Idumea, na katika maeneo yote ng'ambo ya Mto Yordani na yale yanayozunguka Tiro na Sidoni. Lilikuwa kundi kubwa sana la watu. Wote walimjia Yesu kwa sababu walikuwa wamesikia mambo aliyokuwa anafanya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Idumea, ng'ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Idumea, ng'ambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, umati mkubwa wa watu ukamjia kutoka Uyahudi, Yerusalemu, Idumaya, Ng'ambo ya Yordani pamoja na wale wa sehemu za karibu na Tiro na Sidoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, umati mkubwa wa watu ukamjia kutoka Uyahudi, Yerusalemu, Idumaya, na ng’ambo ya Yordani, pamoja na wale wa sehemu za karibu na Tiro na Sidoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na Yerusalemu, na Idumaya, na ng'ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Idumea, ngambo ya mto Yordani, Tiro na Sidoni. Watu hao wengi walimwendea Yesu kwa sababu ya kusikia mambo mengi aliyokuwa ameyatenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
na Yerusalemu na Idumea na ng'ambo ya Yordani na upande wa Tiro na Sidoni, wakamwendea, kwani waliyasikia yote, aliyoyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na Yerusalemu, na Idumaya, na ng’ambo ya Yordani, na pande za Tiro na Sidoni, mkutano mkuu, waliposikia habari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda, wakamwendea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yerusalema, Idumea, katika inchi za upande mwengine wa muto Yordani na pande za muji wa Tiro na wa Sidona. Kundi hili kubwa la watu walimufikia Yesu kwa sababu walisikia habari za mambo aliyofanya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na toka Idumaya, na ngʼambu ya Yardani, na pande za Turo na Sidon, mkutano mkuu, waliposikia khabari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda; wakamwendea.