Mark 3:9 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake watayarishe mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia wanafunzi wake ya kwamba chombo kidogo kikae karibu naye, kwa sababu ya mkutano, wasije wakamsonga.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa sababu ya kundi, aliwaambia wanafunzi wake, kumtayarishia mashua mdogo, ili kwamba wasiweze kumsonga na kumbana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake waweke tayari mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake waweke tayari mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia wanafunzi wake ya kwamba mashua ndogo ikae karibu naye, kwa sababu ya mkutano, wasije wakamsonga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawaambia wanafunzi wake wamtayarishie mashua moja, ili umati wa watu usije ukamsonga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia wanafunzi wake, wamtengenezee chombo kidogo kwa ajili ya makundi ya watu, wasije kumsongasonga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia wanafunzi wake ya kwamba chombo kidogo kikae karibu naye, kwa sababu ya mkutano, wasije wakamsonga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kwa kuona uwingi wa watu wale, Yesu akawaambia wanafunzi wake wamutayarishie chombo kidogo kusudi wasimusonge.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia wanafunzi wake ya kama chombo kidogo kikae karibu nae, kwa sababu ya makutano, wasije wakamsonga.