Mark 4:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wote wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Palikuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekusanyika kumzunguka, hata ikambidi Isa aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkubwa mno, hata yeye akapanda chomboni, akakaa baharini, mkutano wote ulikuwako juu ya nchi kavu kando ya bahari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa mara nyingine Yesu akaanza kufundisha kando ya ziwa. Umati wa watu ukakusanyika kumzunguka, naye akapanda ndani ya mtumbwi ili akae na kufundisha huku mtumbwi ukielea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wote wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umemkusanyikia na kumzunguka ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umekusanyika kumzunguka ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba ilimbidi Isa aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaanza kufundisha tena kando ya ziwa. Kundi kubwa sana la watu wakamkusanyikia, hata yeye akapanda katika mashua, akakaa ziwani, watu wote walikuwa katika nchi kavu kando ya ziwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alianza kufundisha tena akiwa kando ya ziwa. Umati mkubwa wa watu ulimzunguka hata ikambidi aingie katika mashua na kuketi. Watu wote wakawa wamekaa katika nchi kavu, kando ya ziwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaanza tena kufundisha kandokando ya bahari. Wakamkusanyikia kundi la watu wengi mno; kwa hiyo akaingia chomboni, akakaa ufukoni, watu wote wakiwa pwani kandokando ya bahari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkubwa mno, hata yeye akapanda chomboni, akakaa baharini, mkutano wote ulikuwako juu ya nchi kavu kando ya bahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alianza kufundisha tena pembeni ya ziwa la Galilaya. Kundi kubwa la watu walikusanyika karibu naye, kwa hiyo akaingia ndani ya chombo na kuikaa mule. Chombo kilikuwa katika ziwa na watu walisimama inchi kavu, pembeni ya ziwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
AKAANZA kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkuliwa, hatta yeye akapanda chomboni, akakaa baharini; mkutano wote ulikuwako katika inchi kavu kando ya bahari.