Mark 4:15 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengine ni kama walio njiani ambapo neno lilipandwa. Lakini mara tu baada ya kulisikia, Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, mara Shetani huja na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wengine ni kama ile mbegu zilizoanguka juu ya njia pale ambapo neno la Mungu limepandwa. Baada ya kulisikia lile neno la Mungu, ndipo Shetani huja haraka na kuyaondoa yale mafundisho ya Mungu yaliyopandwa ndani yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wengine ni kama wale walio njiani ambapo mbegu zilianguka. Hawa hulisikia hilo neno lakini mara Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengine ni kama walio njiani ambapo neno lilipandwa. Lakini mara tu baada ya kulisikia, Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawa ndio wale walio kando ya njia, ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulichukua lile neno lililopandwa ndani yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengine ni kama walio njiani ambapo neno lilipandwa. Lakini mara tu baada ya kulisikia, Shetani huja na kuliondoa neno hilo lililopandwa ndani yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini zilizoko njiani ndio hao: Neno linapomiagwa, wakiisha kulisikia, papo hapo Satani huja, akaliondoa Neno lililomiagwa mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hawa ndio walio kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nafasi ile mbegu zilipoanguka pembeni ya njia, ni mufano wa watu wanaosikia Neno la Mungu, lakini mara moja Shetani anakuja na kuondoa lile Neno lililopandwa ndani yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hawa ndio walio njiani, lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, marra huja Shetani, akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.