Mark 4:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu walisikiapo hilo neno hulipokea kwa furaha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nazo zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, ni wale wanaolisikia neno, na mara hulipokea kwa furaha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watu wengine ni kama mbegu iliyopandwa kwenye eneo lenye mawe mengi. Wanapolisikia neno wanalipokea haraka kwa furaha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu wanapolisikia hilo neno hulipokea kwa furaha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu walisikiapo hilo neno hulipokea kwa furaha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nazo hizi ni zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, wanapolisikia neno, mara hulipokea kwa furaha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nazo zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, ni wale wanaolisikia neno, na mara hulipokea kwa furaha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengine ni kama zile mbegu zilizopandwa penye mawe. Mara tu walisikiapo hilo neno hulipokea kwa furaha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vilevile zilizomiagwa penye miamba ndio hao: wanapolisikia Neno, papo hapo hulipokea kwa furaha,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, mara hulipokea kwa furaha;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Udongo wenye mawe, pahali mbegu zilipoanguka ni mufano wa watu wanaosikia Neno la Mungu, na mara moja wanalipokea kwa furaha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kadhalika na hawa ndio wapandwao penye mwamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno, marra hulipokea kwa furaha;