Mark 4:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno, mara wanakata tamaa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kwa kuwa hawana mizizi, wao hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, mara wao huiacha imani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini wao wenyewe wanakuwa bado hawajaliruhusu lizame zaidi katika maisha yao. Shida au mateso yanapotokea kwa sababu ya lile neno, kwa haraka sana wanaiacha imani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno mara wanakata tamaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno, mara wanakata tamaa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi kwa kuwa hawana mizizi, hudumu kwa muda mfupi tu, kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, wao mara huiacha imani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kwa kuwa hawana mizizi, wao hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, mara wao huiacha imani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini haliwaingii na kuwa na mizizi ndani yao; huendelea kulizingatia kwa kitambo tu, na wakati taabu au udhalimu vinapotokea kwa sababu ya hilo neno, mara wanakata tamaa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini hawana mizizi mioyoni mwao, ila wanalishika kwa kitambo kidogo tu. Yanapotukia maumivu au mafukuzo kwa ajili ya Neno, mara hujikwaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ila hawana mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa ajili ya lile neno, mara hujikwaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini halizami ndani yao kama mizizi; wanalishika kwa muda mufupi tu. Wakati taabu na mateso vinapowafikia kwa ajili ya Neno la Mungu, mara moja wanaanguka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
waki hawana mizizi ndani yao, hali hudumu muda mehache; kiisha ikitokea shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa.