Mark 4:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwani kila kilichofichika kitafunuliwa, na kila kilicho cha siri kitatokea kweupe kwenye mwanga.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lo lote la siri ambalo halitaletwa nuruni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila kusudi lije kudhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila kusudi lije kutokea wazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kila kilichofichwa kitafichuliwa, na kila kilichofunikwa kitafunuliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hakuna lililofichwa, isipokuwa kwamba lipate kufunuliwa halafu; wala hakuna njama, ila kwamba ipate kutokea waziwazi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni hivi vilevile hakuna chochote kinachofichwa kitakachokosa kuonekana wazi, wala hakuna siri itakayokosa kufunuliwa waziwazi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana hakuna neno lililostirika, illa kusudi lije likadhihirika; wala halikuwa siri, illa kusudi lije likatokea dhahiri.