Mark 4:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akawaambia pia, “Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akawaambia, “Zingatieni kwa makini kile mnachokisikia. Kwani jinsi mnavyosikiliza kwa makini, ndivyo mtakavyoelewa na kuzidi kuelewa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akawaambia pia, “Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akawaambia pia, “Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye akawaambia, “Iweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo mnachotumia kuwapimia wengine, ndicho kitakachotumika kuwapimia ninyi, hata na zaidi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akawaambia pia, “Sikilizeni kwa makini mnachosikia! Kipimo kilekile mnachowapimia watu wengine, ndicho mtakachopimiwa; tena mtazidishiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Mwangalie, jinsi mnavyosikia! Kipimo, mnachokipimia wengine, ndicho, mtakachopimiwa nanyi, tena mtaongezewa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaambia tena: “Muangalie vizuri maneno munayosikia! Mungu atawapimia na kipimo kile munachowapimia wengine, na kuwaongezea hata zaidi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Tafakarini msikialo, kipimo mpimacho mtapimiwa kile kile, na bado mtazidishiwa.