Mark 4:32 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini ikisha pandwa, huota na kuwa mmea mkubwa kuliko mimea yote ya shambani. Matawi yake huwa makubwa hata ndege wa angani huweza kujenga viota vyao katika kivuli chake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikipandwa, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wanaweza kujenga viota kwenye kivuli chake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini inapokuwa imepandwa, inakua na kuwa kubwa sana kuliko mimea yote ya bustanini, na pia hubeba matawi makubwa, kiasi kwamba ndege wa angani wanaweza kupumzika katika kivuli chake.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ikisha pandwa, huota na kuwa mmea mkubwa kuliko mimea yote ya shambani. Matawi yake huwa makubwa hata ndege wa angani huweza kujenga viota vyao katika kivuli chake.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini ikisha pandwa, huota na kuwa mmea mkubwa kuliko mimea yote ya shambani. Matawi yake huwa makubwa hata ndege wa angani huweza kujenga viota vyao katika kivuli chake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani kujenga viota kwenye matawi yake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wanaweza kujenga viota kwenye matawi yake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini ikisha pandwa, huota na kuwa mmea mkubwa kuliko mimea yote ya shambani. Matawi yake huwa makubwa hata ndege wa angani huweza kujenga viota vyao katika kivuli chake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kikiisha pandwa hukua, kiwe mkubwa kuliko miboga yote kwa kuchipuza matawi makubwa, hata ndege wa angani huweza kuja na kutua katika kivuli chake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini ikiisha kupandwa hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikafanya matawi makubwa; hata ndege wa angani waweza kukaa chini ya uvuli wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ikiisha kupandwa, inaota na kuwa kubwa zaidi kuliko mimea yote. Inatoa matawi makubwa hata ndege wanaweza kujenga chicha zao juu yake, kwenye kivuli chake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na ikiisha kupandwa, hukua, ikawa kubwa kuliko miti yote ya mboga, ikifanya matawi makuhwa; hatta ndege za anga waweza kukaa chini ya uvuli wake.