Mark 4:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Vilevile mashua nyingine zilimfuata.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaacha umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua zingine nyingi pamoja naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa hiyo wakaliacha lile kundi. Wakamchukua pamoja nao alipokuwa amerudi katika mtumbwi. Wakati ule ule palikuwepo na mitumbwi mingi mingine ziwani.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Palikuwapo pia mashua nyingine hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Vilevile mashua nyingine zilimfuata.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakiuacha ule umati wa watu nyuma, wakamchukua vile vile kama alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua nyingine nyingi pamoja naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakauacha ule umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua nyingine nyingi pamoja naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyokuwa katika mashua. Na mashua zingine zilikuwako pamoja naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakauacha ule umati wa watu, wakamchukua Yesu katika mashua alimokuwa. Vilevile mashua nyingine zilimfuata.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaliacha kundi la watu, wakamchukua hivyo alivyokuwa chomboni; navyo vyombo vingine vilikuwa pamoja naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wanafunzi wakaaga kundi la watu, wakaingia ndani ya chombo Yesu alimokuwa na kuondoka pamoja naye. Na vyombo vingine vikamusindikiza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakawaacha makutano, wakamchukua vile vile katika chomho kile kile. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja nae.