Mark 4:38 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, “Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
lakini Yesu alikuwa amelala nyuma ya mtumbwi akiegemea mto. Wakamwaamsha na kumwambia, “Mwalimu je wewe hujali kwamba tunazama?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, “Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, “Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alikuwa sehemu ya nyuma ya mashua, amelala juu ya mto. Basi, wanafunzi wakamwamsha na kumwambia, “Mwalimu, je, hujali kwamba sisi tunaangamia?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye alikuwa chomboni upande wa nyuma, amelala usingizi juu ya mto. Ndipo, walipomwamsha wakimwambia: Mfunzi, huoni uchungu, tukiangamia?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alikuwa upande wa nyuma wa chombo, akilala usingizi akilalisha kichwa juu ya mufuko wa kuegemea. Wanafunzi wake wakamwamusha na kumwambia: “Mwalimu, haikuhangaishi kuona sisi tunakufa?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yeye mwenyewe alikuwa katika shetri, amelala juu ya mto: wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunapotea?