Mark 4:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba ikakua, ikaisonga hiyo mimea, hivyo haikutoa mazao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nyingine ikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea ikaisonga, isizae matunda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mbegu nyingine ilianguka kwenye magugu yenye miiba, na miiba ile ilikua na hatimaye kuibana sana na hivyo haikuzaa chochote.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, miiba hiyo ikakua ikaisonga hiyo mimea hivyo haikutoa mazao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba hiyo ikakua, ikaisonga hiyo mimea, hivyo haikutoa mazao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nyingine ikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea ikaisonga, isizae matunda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nyingine zikaangukia penye miiba; nayo miiba ilipoota ikazisonga, zisizae.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nyingine ikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea ikaisonga, isizae matunda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbegu zingine zilianguka katikati ya miiba. Ile miiba ikaota na kuzisonga mbegu hata hazikuweza kutoa kitu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nyingine zikaanguka penye miiba: ile miiba ikakua, ikazisonga, zisizae matunda.