Mark 5:13 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka, wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe wapatao 2,000 likaporomoka kwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani, likatumbukia majini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Isa akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka, wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao elfu mbili, nao wote wakateremkia gengeni kwa kasi, nao wakatumbukia ziwani na kuzama.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye akawaruhusu. Kwa hiyo pepo wachafu walimtoka mtu yule na kuwaingia nguruwe. Kundi lile lilikuwa na idadi karibu ya elfu mbili, lilikimbia kuelekea kwenye kingo zenye mtelemko mkali na kutumbukia ziwani, ambamo walizama.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka, wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe wapatao elfu mbili likaporomoka kwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani, likatumbukia majini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka, wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe wapatao 2,000 likaporomoka kwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani, likatumbukia majini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yesu akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao 2,000, likatelemkia gengeni kwa kasi nalo likazama baharini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Isa akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka, wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao 2,000, nao wote wakateremkia gengeni kwa kasi, nao wakatumbukia ziwani na kuzama.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likateremka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapatao elfu mbili; wakafa baharini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akawaruhusu. Basi, hao pepo wachafu wakatoka, wakawaingia wale nguruwe. Kundi lote la nguruwe wapatao 2,000 likaporomoka kwenye ule mteremko mkali mpaka ziwani, likatumbukia majini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipowapa ruhusa, pepo wachafu wakamtoka, wakawaingia nguruwe; ndipo, kundi lilipotelemka mbio mwambani, wakaingia baharini, wapata kama 2000, wakatoswa baharini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; nalo kundi lote likatelemka kwa kasi gengeni, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaruhusu. Halafu wale pepo wakatoka ndani ya mutu yule na kuingia ndani ya nguruwe. Kundi zima la nguruwe, karibu elfu mbili, wakatelemuka mbio kwenye mulima na kutumbukia ndani ya ziwa, nao wakazama ndani ya maji.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawapa rukhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale ngumwe: kundi lote likatelemka kwa kassi gengeni, wakaingia baharini; walikuwa wapata elfeen; wakafa baharini.