Mark 5:14 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilo mjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliyotukia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watu waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakaenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wale waliowachunga walikimbia. Wakatoa taarifa mjini na katika maeneo jirani ya mashambani. Watu wakaja kuona ni kitu gani kilichotokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilo mjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliyotukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilo mjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliyotukia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakatoka kwenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakatoka kwenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wachungaji wa hao nguruwe walikimbia, wakatangaza jambo hilo mjini na mashambani. Watu wakafika kuona yaliyotukia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wachungaji wao wakakimbia, wakayatangaza mjini na mashambani. Watu wakaja, watazame, lililofanyika lilivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wachungaji wao wakakimbia, wakaieneza habari mjini na mashambani. Watu wakatoka walione lililotokea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wachungaji wa nguruwe wakaenda mbio kupasha habari katika muji na katika vijiji. Watu wakakuja kusudi waone jambo lililotokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wachungaji wa wale nguruwe wakakimbia wakaeneza khahari mjini na mashamba. Wakatoka waone khabari iliyotukia.