Mark 5:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yesu akamkatalia. Badala yake akamwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako, ukawaambie mambo yote Bwana aliyokutendea na jinsi alivyokuonea huruma.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Mwenyezi Mungu, na jinsi alivyokuhurumia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yesu hakumruhusu aende naye, isipokuwa alimwambia, “Nenda kwa watu wa kwenu, na uwaambie yote ambayo Bwana amekufanyia, na uwaambie jinsi alivyokuwa na huruma kwako.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Yesu akamkatalia. Badala yake akamwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako, ukawaambie mambo yote Bwana aliyokutendea na jinsi alivyokuonea huruma.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yesu akamkatalia. Badala yake akamwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako, ukawaambie mambo yote Bwana aliyokutendea na jinsi alivyokuonea huruma.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Bwana na jinsi alivyokuhurumia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Mwenyezi Mungu, na jinsi alivyokuhurumia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Nenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubirie ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yesu akamkatalia. Badala yake akamwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako, ukawaambie mambo yote Bwana aliyokutendea na jinsi alivyokuonea huruma.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hakumwitikia, ila akamwambia: Uende zako nyumbani mwako kwa ndugu zako ukawasimulie yote, Bwana aliyokutendea kwa kukuhurumia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini hakumruhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu hakumuruhusu, lakini akamwambia: “Kwenda kwako kwenye jamaa yako, na uwaelezee mambo Bwana aliyokutendea na namna alivyokuhurumia.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu hakumrukhusu, bali alimwambia, Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawakhubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea Bwana, na jinsi alivyokurehemu.