Mark 5:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alivukia tena upande wa pili wa ziwa kwa mashua. Umati mkubwa wa watu ukakusanyika mbele yake, naye akawa amesimama kando ya ziwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa alipokwisha kuvuka tena na kufika ng’ambo, umati mkubwa wa watu wakamzunguka hapo kando ya bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha, Yesu alivuka kurudi upande wa magharibi wa ziwa. Pale kundi kubwa la watu lilikusanyika kwake. Yeye alikuwa kando ya ziwa, na
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alivukia tena upande wa pili wa ziwa kwa mashua. Umati mkubwa wa watu ukakusanyika mbele yake, naye akawa amesimama kando ya ziwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alivukia tena upande wa pili wa ziwa kwa mashua. Umati mkubwa wa watu ukakusanyika mbele yake, naye akawa amesimama kando ya ziwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu alipokwisha kuvuka tena na kufika ng'ambo, umati mkubwa wa watu ukamzunguka, yeye akiwa kando ya bahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa alipokwisha kuvuka tena na kufika ng’ambo, umati mkubwa wa watu ukamzunguka yeye akiwa hapo kando ya bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng'ambo katika ile mashua, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alivukia tena upande wa pili wa ziwa kwa mashua. Umati mkubwa wa watu ukakusanyika mbele yake, naye akawa amesimama kando ya ziwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipokwisha vuka tena chomboni kuja ng'ambo, kundi la watu wengi likakusanyika hapo, alipokuwa kandokando ya bahari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ng’ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akavuka ngambo ingine ya ziwa la Galilaya. Alipokuwa pembeni ya ziwa, watu wengi wakakusanyika karibu naye.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta Yesu alipokwisha kuvuka kurudia ngʼambu katika kile chombo, wakamkusanyikia makutano mengi: nae alikuwa kando ya bahari.