Mark 5:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa karibu na kufa. Twende tafadhali, ukamwekee mikono yako, apate kupona na kuishi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye ataishi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akamwomba kwa msisitizo, akisema, “Binti yangu mdogo yu karibu kufa. Ninakuomba ufike na kumwekea mikono, ili kwamba apone na kuishi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa karibu kufa. Twende tafadhali, ukamwekee mikono yako, apate kupona na kuishi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa karibu na kufa. Twende tafadhali, ukamwekee mikono yako, apate kupona na kuishi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye atakuwa hai.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yuko karibu kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa karibu na kufa. Twende tafadhali, ukamwekee mikono yako, apate kupona na kuishi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
akambembeleza sana akisema: Kibinti changu yumo kufani; nakuomba, uje, umbandikie mikono, apate kupona na kuwa mzima tena.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
akamusihi sana, akisema: “Binti yangu mudogo yuko karibu kufa. Ninakuomba ukuje kwanza kwa kuweka mikono yako juu yake, kusudi apate kupona na kuishi!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akimsihi sana, akinena. Binti yangu mdogo yu katika kufa: nakuomba nje, nweke mkono wako juu yake, apate kupona, nae ataishi.