Mark 5:30 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alitambua mara kwamba nguvu imemtoka. Basi akaugeukia ule umati wa watu, akauliza, “Nani aliyegusa mavazi yangu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ghafula Isa akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akageukia umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye Yesu akatambua mara moja kwamba nguvu zilimtoka. Aligeuka nyuma na kuuliza “Nani aliyegusa mavazi yangu?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alitambua mara kwamba nguvu imemtoka. Basi akaugeukia ule umati wa watu, akauliza, “Nani aliyegusa mavazi yangu?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alitambua mara kwamba nguvu imemtoka. Basi akaugeukia ule umati wa watu, akauliza, “Nani aliyegusa mavazi yangu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ghafula Yesu akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akaugeukia ule umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyenigusa?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ghafula Isa akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akaugeukia ule umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara Yesu, huku akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alitambua mara kwamba nguvu imemtoka. Basi akaugeukia ule umati wa watu, akauliza, “Nani aliyegusa mavazi yangu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Papo hapo Yesu akatambua mwilini mwake, ya kuwa nguvu imemtoka; akaligeukia kundi la watu, akasema: Yuko nani aliyenigusa nguo zangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mara moja Yesu akatambua kama nguvu zilitoka ndani yake. Basi akageuka kati ya kundi na kuuliza: “Ni nani aliyegusa nguo yangu?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra Yesu akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya makutano, akanena, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?