Mark 5:40 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini wao wakamcheka. Basi, akawatoa wote nje, akawachukua baba yake na mama yake huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale watu wakamcheka. Baada ya kuwafukuza wote nje, Isa akaenda na baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao, wakaingia ndani hadi pale alipokuwa mtoto yule.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nao wakamcheka. Yeye aliwatoa nje watu wote, akamchukua baba na mama wa mtoto na wale waliokuwa pamoja naye, akaenda hadi pale alipokuwepo mtoto,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini wao wakamcheka. Basi, akawaondoa wote nje, akawachukua baba na mama ya huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini wao wakamcheka. Basi, akawatoa wote nje, akawachukua baba yake na mama yake huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale watu wakamcheka kwa dharau. Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao. Wakaingia ndani mpaka pale alipokuwa yule mtoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wale watu wakamcheka kwa dharau. Lakini yeye akawatoa wote nje, akawachukua baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao. Wakaingia ndani mpaka pale alipokuwa yule mtoto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini wao wakamcheka. Basi, akawatoa wote nje, akawachukua baba yake na mama yake huyo msichana na wale wanafunzi wake, wakaingia chumbani alimokuwa huyo msichana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndipo, walipomcheka sana. Lakini alipokwisha kuwafukuza wote akamchukua baba ya kitoto na mama yake na wale waliokuwa pamoja naye, akaingia mle, yule kitoto alimokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wakaanza kumuchekelea. Halafu Yesu akawaondosha wote inje, akawakamata wazazi wa yule mutoto na wanafunzi wake watatu, akaingia katika chumba pahali mutoto alipokuwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa baba yake yule mtoto na mama yake, na wale walio pamoja nae, akaingia ndani alimokuwamo yule mtoto.