Mark 6:10 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena aliwaambia, “Popote mtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humo mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mkiingia kwenye nyumba yoyote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye akawambia, “ikiwa mtu atawapa mahali pa kuishi mkae katika nyumba hiyo kwa muda wote mtakapokuwa katika mji ule msihamehame kutoka nyumba moja hadi nyingine.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena aliwaambia, “Popote mtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humo mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena aliwaambia, “Popote mtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humo mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia, “Mkiingia kwenye nyumba yo yote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia, “Mkiingia kwenye nyumba yoyote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Mahali popote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hadi mtakapotoka mahali pale.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena aliwaambia, “Popote mtakapokaribishwa nyumbani, kaeni humo mpaka mtakapoondoka mahali hapo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Kila mtakamoingia nyumbani, kaeni mwake, mpaka mtakapotoka tena!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hata mtakapotoka mahali pale.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akawaambia tena: “Nafasi yoyote watakapowakaribisha ndani ya nyumba, mubakie mule mpaka mutakapotoka kule.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Mahali po pote mtakapoingia katika nyumba, kaeni humo hatta mtakapotoka mahali pale.