Mark 6:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mahali popote ambapo watu watakataa kuwakaribisheni au kuwasikiliza, ondokeni hapo na kuyakunguta mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mahali popote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kung’uteni mavumbi kutoka miguu yenu ili kuwe ushuhuda dhidi yao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mahali po pote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung'uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu, kuwa ushuhuda kwao.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa hamtakaribishwa ama kusikilizwa katika mji wowote au mahali popote, kwa kuwaonya kunguteni mavumbi toka miguuni mwenu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mahali popote ambapo watu watakataa kuwakaribisheni au kuwasikiliza, ondokeni hapo na kuyakung'uta mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mahali popote ambapo watu watakataa kuwakaribisheni au kuwasikiliza, ondokeni hapo na kuyakung'uta mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mahali po pote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kung'uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mahali popote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kung’uteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mahali popote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung'uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu, kuwa ushuhuda kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mahali popote ambapo watu watakataa kuwakaribisheni au kuwasikiliza, ondokeni hapo na kuyakunguta mavumbi miguuni mwenu kama onyo kwao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo mahali, wasipowapokea, wasiwasikilize, basi, tokeni pale na kuyakung'uta mavumbi yaliyoishika miguu yenu, yaje yanishuhudie kwao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mahali po pote wasipowakaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakung’uteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu, kuwa ushuhuda kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na nafasi yoyote watu watakapokataa kuwakaribisha na kuwasikiliza, mutoke kule na mukungute mavumbi toka juu ya miguu yenu. Jambo hili litakuwa ushuhuda juu yao.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na watu wote wasiokaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakungʼuteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu kuwa ushuhuda kwao.