Mark 6:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Herodia alimchukia sana Yohane, akataka kumuua, asiweze.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwekea Yahya kinyongo, akataka kumuua. Lakini hakuweza,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Herodia alikuwa na kisa na Yohana. Hivyo alitaka auwawe, lakini hakuweza kumshawishi Herode kumuua Yohana.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi Herodia alimchukia sana Yohane, akataka kumwua, asiweze.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Herodia alimchukia sana Yohane, akataka kumuua, asiweze.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwekea Yohana kinyongo akataka kumwua. Lakini hakuweza,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwekea Yahya kinyongo akataka kumuua. Lakini hakuweza,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asiweze.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Herodia alimchukia sana Yohane, akataka kumuua, asiweze.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Herodia alimvizia, akataka kumwua, asiweze.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo Herodia akamuwekea Yoane chuki na kutaka kumwua, lakini hakuweza kwa sababu ya Herode.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi yule Herodias akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate.