Mark 6:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa. Nao wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sinagogi. Watu wengi walishangazwa walipomsikiliza. Wakasema, “Mtu huyu alipata wapi mambo haya? Alipata wapi hekima hii? Na anaifanyaje miujiza hii inayofanyika kwa mikono yake?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi na wengi waliomsikia wakashangaa. Wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa. Nao wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika sunagogi. Wengi waliomsikia walishangaa, wakasema, “Je, ameyapata wapi mambo haya? Ni hekima gani hii aliyopewa? Tena, anatendaje maajabu haya anayoyafanya?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ilipokuwa siku ya mapumziko, akaanza kufundisha katika nyumba ya kuombea, nao wengi waliomsikia wakashangaa, wakasema: Huyu haya ameyapata wapi? Werevu huu ulio wa kweli amepewa na nani? Hizo nguvu nazo zinazotendwa na mikono yake ni nguvu gani?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ilipokuwa sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya Sabato ilipotimia, akaanza kufundisha katika nyumba ya kuabudia. Watu wengi waliomusikiliza, wakashangaa sana na kuulizana: “Huyu amepata maneno haya yote kutoka wapi? Ni hekima ya namna gani aliyopata? Ni kwa uwezo wa namna gani anafanya miujiza kama hii?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ilipokuwa sabato, akaanza kufundisha katika sunagogi: wengi wakisikia, wakashangaa, akinena, Huyu amepata wapi haya? Na, Hekima gani hii aliyopewa huyu, na nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono yake?