Mark 6:21 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo ikapatikana nafasi, wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode. Herode aliwafanyia karamu wazee wa baraza lake, majemadari na viongozi wa Galilaya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hatimaye Herodia alipata wakati mwafaka aliokuwa akiutafuta. Mfalme Herode alifanya karamu kubwa wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake. Akawaalika maafisa wake wakuu, majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini muda maalumu ukafika; katika siku ya kuzaliwa kwake. Herode aliandaa sherehe ya chakula cha jioni kwa maafisa mashuhuri wa baraza lake, maafisa wake wa kijeshi, na watu maarufu wa Galilaya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ikapatikana nafasi, wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode. Herode aliwafanyia karamu wazee wa baraza lake, majemadari na viongozi wa Galilaya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo ikapatikana nafasi, wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode. Herode aliwafanyia karamu wazee wa baraza lake, majemadari na viongozi wa Galilaya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme Herode alifanya karamu kubwa, wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake. Akawaalika maafisa wake wakuu, majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. Hatimaye Herodia alipata wasaa aliokuwa akiutafuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme Herode alifanya karamu kubwa wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake. Akawaalika maafisa wake wakuu, majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. Hatimaye Herodia alipata wasaa aliokuwa akiutafuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo ikapatikana nafasi, wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode. Herode aliwafanyia karamu wazee wa baraza lake, majemadari na viongozi wa Galilaya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku iliyofaa ya kumpata ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode; ndipo, alipowaalika chakulani watawala miji yake na wakubwa wa askari na watu wenye cheo wa Galilea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku moja Herodia alipata wakati wa kumwua Yoane. Ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, wakati alipofanya karamu kwa wasimamizi wa serikali yake, wakubwa wa waaskari na waheshimiwa wa Galilaya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta ilipotokea siku ya kufaa, na Herode (siku kuu ya kuzaliwa kwake) alipowafanyia karamu masheki na majemadari na watu wakubwa wa Galilaya,
Recommended Reading