Mark 6:22 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, binti yake Herodia aliingia, akacheza, akawafurahisha sana Herode na wageni wake. Mfalme akamwambia huyo msichana, “Niombe chochote utakacho, nami nitakupa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Binti Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani. Mfalme Herode akamwambia yule binti, “Niombe kitu chochote utakacho, nami nitakupa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Binti ya Herodia alipowasili ndani ya ukumbi alicheza na kumpendeza Herode na wageni aliowaalika katika sherehe hiyo. Mfalme Herode akamwambia yule msichana, “Uniombe chochote unachotaka, nami nitakupa.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, binti yake Herodia aliingia, akacheza, akawafurahisha sana Herode na wageni wake. Mfalme akamwambia huyo msichana, “Niombe chochote utakacho, nami nitakupa.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, binti yake Herodia aliingia, akacheza, akawafurahisha sana Herode na wageni wake. Mfalme akamwambia huyo msichana, “Niombe chochote utakacho, nami nitakupa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Binti yake Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani. Mfalme Herode akamwambia yule binti, “Niombe kitu cho chote utakacho, nami nitakupa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Binti yake Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani. Mfalme Herode akamwambia yule binti, “Niombe kitu chochote utakacho, nami nitakupa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lolote utakalo, nitakupa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, binti yake Herodia aliingia, akacheza, akawafurahisha sana Herode na wageni wake. Mfalme akamwambia huyo msichana, “Niombe chochote utakacho, nami nitakupa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Binti Herodia alipoingia na kucheza ngoma, akampendeza Herode na wale waliokaa pamoja naye chakulani. Ndipo, mfalme alipomwambia huyo msichana:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo binti yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Binti ya Herodia aliingia na kucheza hata Herode na waalikwa wake wakapendezwa. Halafu mufalme akamwambia yule binti: “Uniombe kitu chochote unachotaka, nami nitakupa.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
ndipo binti yake yule Herodias akaingia, akacheza, akampendeza Herode nao walioketi pamoja nae karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lo lote utakalo, nitakupa.