Mark 6:48 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji, akataka kuwapita.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye akawaona wanafunzi wake wakihangaika kupiga makasia, kwani upepo uliwapinga. Kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi Yesu aliwaendea akitembea juu ya ziwa. Yeye akiwa karibu kuwapita,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea akitembea juu ya maji. Alitaka kuwapita.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji, akataka kuwapita.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Karibu na mapambazuko, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akitembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa unwakabili; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, akawaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kupiga makasia, maana upepo ulikuwa unawapinga. Karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji, akataka kuwapita.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaona, wakihangaishwa, wasiweze kwendelea, kwani upepo uliwatokea mbele. Ilipofika zamu ya nne ya usiku, akawajia akienda juu ya bahari, akataka kuwapita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaona wakitaabika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hata ilipopata kama zamu ya nne ya usiku akawaendea, akitembea juu ya bahari; akataka kuwapita.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliwaona wanafunzi wake wakitaabika kwa kuendesha chombo sababu upepo ulikuwa ukiwarudisha nyuma. Basi ilipokuwa karibu na mapambazuko, Yesu akawafikia akitembea juu ya maji, akitaka kuwapita.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaona wakitaahika kwa kuvuta makasia, kwa maana upepo ulikuwa wa mbisho; hatta yapata zamu ya nne ya usiku akawaendea akitemhea juu ya bahari; akataka kuwdpita.