Mark 6:50 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Isa akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa kuwa wote walimwona, na wakaogopa. Mara tu alizungumza nao na kuwaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Usiogope.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni Mimi, msiogope!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa sababu wote walipomwona waliogopa. Mara Isa akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana wote walipomwona waliogopa sana. Mara Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwani wote walimwona, wakatetemeka. Papo hapo yeye akasema nao akawaambia: Tulieni! Ni miye, msiogope!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa maana wote walimwona na kuogopa sana. Lakini mara moja Yesu akasema nao na kuwaambia: “Mujipe moyo, ni mimi! Musiogope!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Marra akasema nao, akawaambia, Jipeni moyo: ni mimi msiogope.