Mark 7:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nyinyi mwafundisha, ‘Kama mtu anacho kitu ambacho angeweza kumsaidia nacho baba yake au mama yake, lakini akasema kwamba kitu hicho ni Korbani (yaani zawadi kwa Mungu),
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia ni Korbani’ (yaani kimewekwa wakfu kwa Mungu),
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ikiwa mtu atamwambia baba au mama yake, ‘Nilikuwa na kitu ambacho ningekupa kikusaidie, lakini nimeahidi kukitoa wakfu kwa Mungu, nacho sasa ni kurbani. ’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ninyi mwafundisha, Kama mtu anacho kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema kwamba kitu hicho ni Korbani (yaani ni zawadi kwa Mungu),
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nyinyi mwafundisha, ‘Kama mtu anacho kitu ambacho angeweza kumsaidia nacho baba yake au mama yake, lakini akasema kwamba kitu hicho ni Korbani (yaani zawadi kwa Mungu),
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninyi mwasema mtu akimwambia baba yake au mama yake kuwa, ‘Msaada ambao ningekupa ni Korbani’ (yaani, umetengwa kama sadaka kwa Mungu),
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia ni Korbani’ (yaani kimewekwa wakfu kwa Mungu),
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu chochote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nyinyi mwafundisha, ‘Kama mtu anacho kitu ambacho angeweza kumsaidia nacho baba yake au mama yake, lakini akasema kwamba kitu hicho ni Korbani (yaani zawadi kwa Mungu),
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi husema: Mtu akimwambia baba au mama: Korbani, ni kwamba: Mali, unazozitaka, nikusaidie nazo, amepewa Mungu, basi, ni vema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, Ni Korbani, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi munasema kwamba mutu akiwa na kitu cha kumusaidia baba au mama yake, lakini akimwambia kwamba kitu kile ni Korbane, (maana yake, kimetolewa kuwa sadaka takatifu kwa Mungu),
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali ninyi hunena, Mtu akimwambia baba yake au mama yake, Ni Korban (yaani kimewekwa wakfu) kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho: