Mark 7:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye akawaambia, “Je, hata nyinyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu kutoka nje, hakiwezi kumtia unajisi,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawajibu, “Je, hata nanyi hamwelewi? Je, hamfahamu kwamba kitu kimwingiacho mtu hakimtii unajisi?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na akawaambia, “Hata nanyi hamuelewi pia? Je, hamuelewi ya kuwa hakuna kinachomwingia mtu kutoka nje kinachoweza kumchafua mtu?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Naye akawaambia, “Je, hata ninyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu toka nje hakiwezi kumtia unajisi,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye akawaambia, “Je, hata nyinyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu kutoka nje, hakiwezi kumtia unajisi,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawajibu, “Hata nanyi hamwelewi? Hamtambui kwamba kitu kimwingiacho mtu hakimtii unajisi?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawajibu, “Je, hata nanyi hamwelewi? Je, hamfahamu kwamba kitu kimwingiacho mtu hakimtii unajisi?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye akawaambia, “Je, hata nyinyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu kutoka nje, hakiwezi kumtia unajisi,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Kumbe nanyi hamjaerevuka hata leo! Hamjui, kila kitu kilichoko nje kikiingia ndani ya mtu hakiwezi kumtia uchafu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akawaambia: “Hata ninyi vilevile hamuwezi kuelewa? Hamufahamu kwamba kila kitu kinachoingia ndani ya mutu kutoka inje hakiwezi kumuchafua?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawaambia, Hivi na ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kuwa killa kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia najis;