Mark 7:24 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu aliondoka hapo, akaenda wilaya ya Tiro. Huko aliingia katika nyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza kujificha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Isa akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akaondoka mahali pale na kuenda katika eneo lililozunguka Tiro. Aliingia katika nyumba na hakutaka mu yeyote ajue hilo, lakini hakuweza kufanya siri kuwepo kwake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu aliondoka hapo, akaenda hadi wilaya ya Tiro. Huko aliingia katika nyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza kujificha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu aliondoka hapo, akaenda wilaya ya Tiro. Huko aliingia katika nyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza kujificha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu ye yote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Isa akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu aliondoka hapo, akaenda wilaya ya Tiro. Huko aliingia katika nyumba moja na hakutaka mtu ajue; lakini hakuweza kujificha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoondoka pale, akaenda mipakani kwa Tiro, akaingia nyumbani, maana alitaka, asijulikane na mtu, lakini hakuweza kufichika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaondoka huko, akaenda zake hata mipaka ya Tiro na Sidoni. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kusitirika.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akaondoka pale, na kwenda katika jimbo lililokuwa karibu na muji Tiro. Akaingia ndani ya nyumba, naye hakutaka mutu ajue kwamba yuko mule, lakini haikuwezekana kwake kujificha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaondoka huko, akaenda zake hatta mipaka ya Turo na Sidon. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kustirika.