Mark 7:25 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwa na pepo, alisikia habari za Yesu. Basi, akaja akajitupa chini mbele ya miguu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwa na pepo mchafu mara moja akasikia juu ya Yesu hivyo alimwijia na kuanguka chini yake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwa na pepo, alisikia habari za Yesu. Basi, akaja akajitupa chini mbele ya miguu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwa na pepo, alisikia habari za Yesu. Basi, akaja akajitupa chini mbele ya miguu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mwanamke mmoja ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ila mara mwanamke, ambaye binti yake ana pepo mchafu, alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo mwanamke mmoja ambaye binti yake alikuwa na pepo, alisikia habari za Yesu. Basi, akaja akajitupa chini mbele ya miguu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani papo hapo mwanamke alisikia, ya kuwa yuko. Kwa kuwa na mtoto mwenye pepo mchafu akaja, akamwangukia miguuni pake;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ila mara mwanamke, ambaye binti yake yuna pepo mchafu, alisikia habari zake, akaja akamwangukia miguuni pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanamuke mumoja, binti yake aliyeshikwa na pepo, akasikia habari za Yesu. Mara moja akamufikia Yesu na kujitupa kwa miguu yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu mwanamke, ambae binti yake yuna pepo mchafu, alisikia khabari zake, akaja akamwangukia miguu.