Mark 7:28 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini huyo mama akasema, “Ni kweli, Bwana; lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini yule mwanamke akamjibu, “Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini yeye akajibu, “Bwana hata mbwa walio chini ya meza wanakula mabaki ya chakula cha watoto.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini huyo mama akasema, “Sawa, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini huyo mama akasema, “Ni kweli, Bwana; lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini yule mwanamke akamjibu, “Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini yule mwanamke akamjibu, “Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini huyo mama akasema, “Ni kweli, Bwana; lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akamjibu akisema: Ndio, Bwana, lakini nao vijibwa hula chini ya meza makombo ya vitoto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanamuke yule akamujibu: “Bwana, unasema ukweli, lakini hata imbwa wanazoea kula makombo watoto wanayoyaangusha chini ya meza.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae akajibu, akamwambia, Naam, Bwana, lakini hatta mbwa chini ya meza hula makombo ya watoto.