Mark 7:31 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yesu aliondoka wilaya ya Tiro, akapitia Sidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Isa akaondoka sehemu za Tiro, akapita katikati ya Sidoni, hadi Bahari ya Galilaya na kuingia eneo la Dekapoli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akarudi kutoka katika eneo kuzunguka jiji la Tiro na akapita katika jiji la Sidoni hadi Ziwa Galilaya akipita katika jimbo la Dekapoli.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha Yesu aliondoka wilayani Tiro, akapitia Sidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yesu aliondoka wilaya ya Tiro, akapitia Sidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yesu akaondoka sehemu za Tiro, akapita katikati ya Sidoni, hadi Bahari ya Galilaya na kuingia eneo la Dekapoli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Isa akaondoka sehemu za Tiro, akapita katikati ya Sidoni, hadi Bahari ya Galilaya na kuingia eneo la Dekapoli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka ziwa la Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yesu aliondoka wilaya ya Tiro, akapitia Sidoni, akafika ziwa Galilaya kwa kupitia nchi ya Dekapoli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Alipotoka tena mipakani kwa Tiro akapita Sidoni, akafika kwenye bahari ya Galilea katikati ya mipaka ya ile Miji Kumi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatoka tena katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yesu akaondoka kule katika jimbo lililokuwa karibu na Tiro, akapita Sidona na katikati ya inchi ya Miji Kumi, hata akafika kwenye ziwa la Galilaya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akatoka tena katika mipaka ya Turo akapita katikati ya Sidon, akaenda hatta bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli.