Mark 7:32 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakamletea bubu kiziwi, wakamwomba amwekee mikono.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huko, watu wakamletea Isa mtu mmoja kiziwi, ambaye pia alikuwa na kigugumizi, wakamwomba aweke mkono wake juu ya huyo mtu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Pale watu wengine wakamletea mtu asiyeweza kusikia na tena aliyesema kwa shida. Nao wakamwomba Yesu amwekee mikono yake na kumponya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakamletea bubu-kiziwi, wakamwomba amwekee mikono.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakamletea bubu kiziwi, wakamwomba amwekee mikono.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huko, watu wakamletea Yesu mtu mmoja kiziwi, ambaye pia alikuwa na kigugumizi, wakamwomba aweke mkono wake juu ya huyo mtu na amponye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huko, watu wakamletea Isa mtu mmoja kiziwi, ambaye pia alikuwa na kigugumizi, wakamwomba aweke mkono wake juu ya huyo mtu na amponye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakamletea bubu kiziwi, wakamwomba amwekee mikono.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamletea mtu aliyekuwa kiziwi na bubu, wakambembeleza, ambandikie mkono.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamuletea mutu mumoja aliyekuwa kiziwi na mwenye kigugumizi vilevile. Wale waliomuleta wakamusihi Yesu amuponyeshe kwa kuweka mikono juu yake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamletea kiziwi, nae ana kigugumizi, wakamsihi aweke mikono yake juu yake.