Mark 7:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, hawali kitu chochote kutoka sokoni, mpaka wamekiosha kwanza. Kuna pia desturi nyingine walizozipokea toka zamani kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuria na vyombo vya shaba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi zingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu na vyombo vya shaba.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na wanaporudi kutoka sokoni, hawali chakula kwanza mpaka wamenawa. Na zipo desturi nyingi wanazozishika, kama vile kuosha vikombe, magudulia na mitungi ya shaba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena hawali kitu chochote kutoka sokoni mpaka wamekiosha kwanza. Kuna pia desturi nyingine walizopokea kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuria na vyombo vya shaba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, hawali kitu chochote kutoka sokoni, mpaka wamekiosha kwanza. Kuna pia desturi nyingine walizozipokea toka zamani kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuria na vyombo vya shaba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi nyingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu na vyombo vya shaba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi nyingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu na vyombo vya shaba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena wakitoka sokoni, wasiponawa, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, hawali kitu chochote kutoka sokoni, mpaka wamekiosha kwanza. Kuna pia desturi nyingine walizozipokea toka zamani kama vile namna ya kuosha vikombe, sufuria na vyombo vya shaba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Navyo vya sokoni hawavili, wasipoviosha kwanza; nayo mambo mengine mengi yako, waliyoyapokea kuyashika, kama kuosha vinyweo na mitungi na vyungu na vitanda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, wanapotoka kwa soko, hawakuli pasipo kuoga kwanza. Na zaidi ya hii wanashika desturi zingine nyingi kama vile namna ya kusafisha vikombe, mitungi na vyungu vilivyotengenezwa na shaba.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyushika kama vile kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba na meza.