Mark 8:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wakati ule nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa watu 5,000? Mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki.” Wakamjibu, “Kumi na viwili.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipoimega ile mikate mitano kwa watu elfu tano, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa mabaki?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nilipoivunja ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Kumi na viwili.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Nilipomega na kugawa mikate mitano kwa watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa masalia ya mikate?” Wakasema “Kumi na viwili”.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
wakati ule nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa watu elfu tano? Mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki ya makombo?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wakati ule nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa watu 5,000? Mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki.” Wakamjibu, “Kumi na viwili.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipoimega ile mikate mitano kuwalisha watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipoimega ile mikate mitano kuwalisha watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilipoivunja ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Kumi na viwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wakati ule nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa watu 5,000? Mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki.” Wakamjibu, “Kumi na viwili.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala hamwikumbuki ile mikate mitano, nilipoimegea wale 5000? Hapo mlijaza makapo mangapi mkiokota makombo? Wakamwambia: Kumi na mawili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nilipoivunja ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Kumi na viwili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wakati nilipomega mikate mitano na kulisha watu elfu tano? Wakati ule mulijaza vitunga ngapi na vipande vya mikate?” Wakajibu: “Kumi na viwili.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nilipoimega ile mikate mitano na kuwapa wale elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Thenashara.