Mark 8:20 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Na nilipoimega ile mikate saba na kuwapa watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki?” Wakamjibu, “Saba.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Je, nilipoimega ile mikate saba kwa watu elfu nne, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa mabaki?” Wakamjibu, “Saba.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Nilipomega na kugawa mikate saba kwa watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa masalia ya mikate?” Wakasema “Saba”.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Na nilipoimega ile mikate saba na kuwapa watu elfu nne, mlikusanya makapu mangapi ya makombo?” Wakamjibu, “Saba.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Na nilipoimega ile mikate saba na kuwapa watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki?” Wakamjibu, “Saba.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Je, nilipomega ile mikate saba kuwalisha watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?” Wakamjibu, “Saba.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Je, nilipoimega ile mikate saba kuwalisha watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa vya masazo?” Wakamjibu, “Saba.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua vikapu vingapi vimejaa vipande? Wakamwambia, Saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Na nilipoimega ile mikate saba na kuwapa watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vya mabaki?” Wakamjibu, “Saba.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wala hamwikumbuki ile mikate saba, nilipoivunjia wale 4000, mlijaza makanda mangapi mkiokota makombo? Wakamwambia: Saba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye akawauliza tena: “Na wakati nilipomega mikate saba na kulisha watu elfu ine, mulijaza vitunga ngapi na vipande vya mikate?” Wakamujibu: “Saba.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ile saba kuwapa wale elfu nne, mlichukua makanda mangapi yamejaa vipande? Wakamwambia, Saba.