Mark 8:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamshika huyo kipofu mkono, akampeleka nje ya kijiji. Akamtemea mate machoni, akamwekea mikono, akamwuliza, “Je, unaweza kuona kitu?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Isa akamuuliza, “Unaona chochote?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alimshika mkono yule asiyeona na kumtoa nje ya kijiji. Kisha Yesu alimtemea mate yule asiyeona kwenye macho yake, akaweka mkono wake juu ya asiyeona, na kumwuliza, “Je! Unaona kitu chochote?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamshika mkono huyo kipofu, akampeleka nje ya kijiji. Akamtemea mate machoni, akamwekea mikono, akamwuliza, “Je, unaweza kuona kitu?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamshika huyo kipofu mkono, akampeleka nje ya kijiji. Akamtemea mate machoni, akamwekea mikono, akamwuliza, “Je, unaweza kuona kitu?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamwuliza, “Unaona cho chote?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Isa akamuuliza, “Unaona chochote?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate katika macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamshika huyo kipofu mkono, akampeleka nje ya kijiji. Akamtemea mate machoni, akamwekea mikono, akamwuliza, “Je, unaweza kuona kitu?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaushika mkono wa kipofu, akamwongoza, watoke kijijini, akamtemea mate machoni, akambandikia mikono, akamwuliza: Kiko, unachokiona?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akashika mukono wa yule kipofu na kumupeleka inje ya kijiji. Yesu alipokwisha kupakaa mate kwa macho ya mutu yule na kuweka mikono juu yake, akamwuliza: “Unaona kitu?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamshika mkono vule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate ya macho, akaweka mikono yake juu yake, akamwuliza, Waona kitu?