Mark 9:1 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akaendelea kuwaambia, “Kweli nawaambieni, wako wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa enzi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akaendelea kuwaambia, “Amin, nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Naye Yesu aliwaambia, “Ninawaambia Ukweli: baadhi yenu mnaosimama hapa mtauona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu kabla ya kufa kwenu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akaendelea kuwaambia, “Kweli nawaambieni, wako wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa enzi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akaendelea kuwaambia, “Kweli nawaambieni, wako wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa enzi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akaendelea kuwaambia, “Amin, amin nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija katika nguvu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akaendelea kuwaambia, “Amin, nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mwenyezi Mungu ukija kwa nguvu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akaendelea kuwaambia, “Kweli nawaambieni, wako wengine papa hapa ambao hawatakufa kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa enzi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia: Kweli nawaambiani: Miongoni mwao wanaosimama hapa wamo wengine, ambao hawatakuonja kufa, mpaka watakapouona ufalme wa Mungu, ukiisha kuja kwa nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na Yesu akaongeza kusema: “Kweli ninawaambia: wamoja kati ya watu wanaokuwa hapa hawatakufa mbele hawajaona Ufalme wa Mungu ukikuja kwa uwezo.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
AKAWAAMBIA, Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa ambao hawataonja mauti hatta watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.