Mark 9:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo mtu mmoja katika ule umati wa watu akamjibu, “Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo aliyemfanya kuwa bubu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu mmoja miongoni mwa umati ule wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na mtu mmoja kundini alimjibu, “Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako ili umponye. Yeye amefungwa na pepo mbaya anayemfanya asiweze kuzungumza.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo mtu mmoja katika ule umati wa watu akamjibu, “Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo aliyemfanya kuwa bubu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo mtu mmoja katika ule umati wa watu akamjibu, “Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo aliyemfanya kuwa bubu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anamfanya asiweze kuongea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtu mmoja miongoni mwa ule umati wa watu akajibu, “Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo mtu mmoja katika ule umati wa watu akamjibu, “Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo aliyemfanya kuwa bubu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmoja wao wale watu wengi akamjibu: Mfunzi, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo wa ububu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu mmoja katika mkutano akamjibu, Mwalimu, nimemleta mwanangu kwako, ana pepo bubu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na mutu mumoja kati ya kundi akamujibu: “Mwalimu, nimemuleta mwana wangu kwako, kwa maana yuko na pepo wa bubu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu mmoja katika makutano akamjibu, Nalimieta mwana wangu kwako, ana pepo bubu: