Mark 9:2 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu peke yao. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya siku sita, Isa akawachukua Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Isa akageuka sura mbele yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Baada ya siku sita, Yesu akamchukua Petro, Yakobo na Yohana na kuwaongoza hadi mlima mrefu wakiwa peke yao tu. Na mwonekano wa Yesu ulibadilika mbele yao. Huko Yesu akabadilika sura nyingine akiwa mbele yao.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu peke yao. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu peke yao. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya siku sita, Isa akawachukua Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Isa akageuka sura mbele yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu peke yao. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Baada ya siku sita Yesu akamchukua Petero na Yakobo na Yohana, akapanda pamoja nao peke yao pasipo watu wengine juu ya mlima mrefu. Huko akageuzwa sura yake machoni pao,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya siku sita, Yesu aliwatwaa Petro, Yakobo na Yoane, na kuwapeleka kwenye mulima murefu pekee yao. Na kule sura ya Yesu ikageuka mbele yao.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, na Yakobo, na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu kwa faragha peke yao: