Mark 9:26 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo huyo pepo alipaza sauti, akamwangusha huyo mtoto chini, kisha akamtoka. Mtoto alionekana kama maiti, hata wengine walisema, “Amekufa!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya yule pepo mchafu kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, “Amekufa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Na pepo yule alilia kwa sauti, akamtupa yule mvulana chini katika mishituko ya kutisha, kisha akatoka, naye akawa kama mtu aliyekufa, kiasi kwamba watu wengi wakadhani ya kuwa amekufa.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo huyo pepo alipaaza sauti, akamwangusha huyo mtoto chini, kisha akamtoka. Mtoto alionekana kama maiti, hata wengine walisema, “Amekufa!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo huyo pepo alipaza sauti, akamwangusha huyo mtoto chini, kisha akamtoka. Mtoto alionekana kama maiti, hata wengine walisema, “Amekufa!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule pepo mchafu akiisha kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, “Amekufa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule pepo mchafu akiisha kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, na akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, “Amekufa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo huyo pepo alipaza sauti, akamwangusha huyo mtoto chini, kisha akamtoka. Mtoto alionekana kama maiti, hata wengine walisema, “Amekufa!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipolia, akamsukumasukuma kwa nguvu, akamtoka; naye akawa kama mfu, hata wengi wakasema: Amekufa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yule pepo akalalamika, akamutikisatikisa mutoto kwa nguvu na kutoka ndani yake. Mutoto akaonekana sawa amekufa, hata watu wengi wakaanza kusema kwamba amekufa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akalia, akamrarua sana, akamtoka: akawa kama amekufa: hatta wengi wakasema, Amekufa.