Mark 9:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mavazi yake yakangaa, yakawa meupe sana, jinsi dobi yeyote duniani asingeweza kuyafanya meupe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko vile mtu yeyote duniani angeweza kuyang’arisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mavazi yake yakimeta-meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mavazi yake yakiwa na mng'ao, na meupe kabisa kuliko mtu anavyoweza kufua nguo kwa sabuni na kuitakatisha.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
mavazi yake yakang'aa, yakawa meupe sana, jinsi dobi yeyote duniani asingeweza kuyafanya meupe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mavazi yake yakang'aa, yakawa meupe sana, jinsi dobi yeyote duniani asingeweza kuyafanya meupe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu ye yote duniani angaliweza kuyang'arisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyang’arisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mavazi yake yakimetameta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mavazi yake yakangaa, yakawa meupe sana, jinsi dobi yeyote duniani asingeweza kuyafanya meupe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nazo nguo zake zikawa nyeupe sana, zikamerimeta; nchini hakuna fundi anayeweza kuzing'aza hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mavazi yake yakimeta-meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nguo zake zikageuka nyeupe sana na kumetameta, wala katika dunia hakuna fundi wa kufua anayeweza kuziangarisha kama vile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akageuka sura yake mbele yao: mavazi yake yakawa yakimetameta, meupe kwa mfano wa thuluji, jinsi asivyoweza fundi duniani kuyafanya meupe.