Mark 9:37 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Anayempokea mtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule aliyenituma.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Yeyote atakayemkaribisha mtoto mdogo kama huyu hapa kwa sababu ya jina langu basi ananikaribisha na mimi pia. Yeyote anayenikubali mimi hanikubali mimi tu bali anamkubali pia yeye aliyenituma.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Anayempokea mtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule aliyenituma.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Anayempokea mtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule aliyenituma.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mtu ye yote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo, kwa Jina langu anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Anayempokea mtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule aliyenituma.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu atakayepokea kitoto mmoja aliye kama huyu kwa Jina languhunipokea mimi. Tena mtu akinipokea mimi hanipokei mimi, ila humpokea yule aliyenituma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Anayemupokea mutoto mudogo kama huyu kwa ajili yangu, ananipokea mimi. Na anayenipokea, hanipokei mimi tu, lakini anamupokea vilevile yule aliyenituma.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtu akimpokea kitoto kimoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi: na mtu akinipokea mimi, hanipokei mimi, bali yeye aliyenituma.